Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa taarifa hiyo, washambuliaji walitokea ndani ya Afghanistan na kushambulia kituo cha askari wa mpakani na kuua askari wasiopungua watano wa Pakistan.
Taarifa hiyo imesema, hii ni mara ya pili kutokea tukio kama hilo kwenye mpaka wa Pakistan na Afghanistan tangu liliporejea madarakani kundi la Taliban nchini Afghanistan.
Jeshi la Pakistan limesema kuwa, limetoa majibu makali kwa washambuliaji hao ndani ya ardhi ya Afghanistan na kuwasababishia hasara kubwa.
Jeshi la Pakistan limesema kuwa, watu hao wenye silaha wamevuuka mpaka wa Afghanistan na kuingia ndani ya ardhi ya Pakistan na baadaye kufyatua risasi na kuua askari watano wa kituo cha Kwaram ndani ya Pakistan.
Shirika la habari la Reuters limesema kuwa, kundi la Tahrik Taliban Pakistan ambalo limeungana tena na kundi la Taliban la Afghanistan baada ya kuchukua madaraka nchini humo, ndilo lililotangaza kuhusika na mauaji ya askari hao watano wa Pakistan.
Mwaka jana Taliban ya Afghanistan ilikuwa na nafasi kubwa katika kufanikisha mazungumzo baina ya Taliban ya Pakistan na serikali ya Islamabad.
Hata hivyo mazungumzo hayo yalikwama baada ya Taliban ya Pakistan kushambulia askari wa Pakistan katika mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.
342/